Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)

 1. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Hisia za wagombea wengine baada ya Dkt Hussein Mwinyi kutangazwa mshindi

  Dkt Hussein Mwinyi
  Image caption: Dkt Hussein Mwinyi rais mteule wa Zanzibar

  Baada ya Tume ya uchaguzi Zanzibar kumtangaza Dkt Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa urais Zanzibar, wafuasi wake wa chama cha Mapinduzi walipokea ushindi huo kwa furaha na shangwe.

  Lakini je wapinzani wake wamepokea vipi matokeo hayo?

  Hapo jana kulipoanza kuonesha dalili kuwa Dkt Hussein Mwinyi anaelekea kushinda, chama kikuu cha upinzani kikiongozwa na mwenyekiti wake na aliyekuwa mgombea urais Maalim Seif Sharif kupitia chama cha ACT Wazalendo, wao walizungumza na waandishi wa habari wakiashiria kupinga matokeo hayo kiasi cha kujitokeza barabarani kutaka kuandamana.

  Lakini baadhi ya viongozi wengine wa upinzani walisema wameridhia ushindi wa Dkt Mwinyi na kuahidi kumpa ushirikiano.

  Juma Ali Khatib kupitia chama cha ADA TADEA alisema kuwa yeye na chama chake wameridhika.

  ‘’Sasa ni wakati wa kufanya kazi na kujenga nchi yetu.’’

  Hamad Muhammed Ibrahim mgombea urais wa chama cha UPDP alisema:

  ‘’Matokeo haya mimi nasema ni maamuzi ya Wazanzibari, mimi kama mgombea kutoka UPDP nitashirikiana naye wakati wowote.’’

  Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia Makini, Ameri Said Ameri yeye anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumaliza uchaguzi salama na kwa amani na ameahidi kushirikiana na Dkt Hussein Mwinyi ili kuhakikisha maendeleo ya Zanzibar yanapatikana.

 2. Dkt Hussein Mwinyi ni rais mteule wa Zanzibar

  Safari yake kisiasa ilianzia mwaka 2000, alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga kwa upande wa Tanzania bara, na kisha mwaka 2005 kuhamia upande wa Zanzibar katika jimbo la Kwahani ambalo ameliongoza kwa miaka 15.

  Soma Zaidi
  next